Habari za Mastaa

Headlines za Kylie Jenner kurudiana na Tyga za pamba moto baada ya kuachana na Travis Scott

on

Baada ya kusambaa kwa taarifa za kuachana kwa Kylie Jenner na aliyekuwa mpenzi wake Travis Scott, Kylie ameonekana tena na Tyga kwenye kumbi wa Hyde Lounge huko West Hollywood usiku wa jumamosi ambapo kupitia mtandao wa TMZ Kylie Jenner alionekana akiwa anaingia kwenye ukumbi huo ambao pia Tyga alikuwepo ndani.

Imeripotiwa kuwa licha ya kwamba Kylie Jenner kuonekana maeneo hayo bado pia alikuwa ni mtu wa furaha muda wote aliokuwa kwenye ukumbi huo na hii inakuwa ni mara ya pili Kylie kuonekana eneo moja na mpenzi wake wa zamani Tyga ikiwa ni siku chache tu baada ya Kuachana na Travis Scott.

Mara ya kwanza kwa wawili hao kuonekana ilikuwa ni wiki iliyopita Kylie alionekana tena akiingia kwenye studio alizokuwa ananitumia Tyga pia usiku huo huo.

Bonyeza PLAY kwenye video hapa chini

Soma na hizi

Tupia Comments