Rapper Nikk Mbishi ameamua kuwatolea uvivu wasanii wa hip hop ambao ni Mon Centrozone na Country Boy ambao wameonekana kuwa tofauti kidogo baada ya Moni Centrozone kuonekana na kikuku huku Country Boy akionekana na lipstick kwenye mdomo.
Sasa Nikki Mbishi akamua kuwaandikia haya …>>>”Dada mwenye mimba leo mtoto wako atakuta UPUUZI tu akizaliwa, atakuta wanaume wanavaa vikuku kama MONI na kupaka lipstick kama COUNTRY BOY eti ndo HIP HOP ya leo, MUZIKI tulisikiliza SISI.
“Hamna hata nguvu kiushawishi kwamba mnaweza kuwa ROLE MODELS, mzazi gani atapenda mwanae aige UCHO**O wa lipstick na vikuku kwa watoto wake wa kiume, tunajua hamjali kitu basi hata WAZAZI wenu.” – Nikki Mbishi
Baada ya Nikki Mbishi kupost hayo kwenye ukurasa wake wa Twitter, naye msanii Young Lunya akaamua kuingilia kati kwa kudai kuwa Nikki Mbishi anakosea sana kwani badala ya kuwa- support yeye amekuwa akiwakosoa kwa kila kitu….
>>>>“Bro Kwanini Umekuwa Kaka wa Kudiss Vijana Wadogo na sio Kusapoti? Unaonaje huo mda unaotumia Kudiss Uutumie Kusapoti kazi Za Vijana Wenzio @countryboytz moni_centrozone wana Ngoma Mpya, Ungetumia huo mda wa kuwadiss kuwasaidia kupromote kazi zao na sio kuharibu..Mimi Binafsi Nakuheshimu na kukukubali sanaa Ila Unanikwaza sanaa Nnapoona Baada Ya Kusapoti unadiss
..”Sasa Unawafundisha nini Wasanii wanaokutazama?? Kama sio Chuki tuu Tumia Acc yako Kusapoti kazi za wadogo zako kaka Mambo ya Kudiss Tuwaachie wenye Acc za Udaku. nikkimbishi nikkimbishi Badilika Bro Jiwe Jipya La nikkimbishi onetheincredible na stereosingasinga Limetoka link kwenye Bio yako Twende kaziiii” – Young Lunya
VIDEO: Tazara imenoga ishakamilika asilimia 90