Ajali

Wizi kutokea eneo la ajali sio kwa Bongo pekeyake, imemkuta na huyu mama Marekani.. +Pichaz

on

Kwenye matukio ya ajali wizi nao huwa unakuwepo, yani mfano imetokea ajali wapo wanaokuja kwa lengo la kusaidia majeruhi wa ajali, lakini wapo wanaokuja na malengo na maslahi yao mengine kabisa tena bila hata kutoa msaada wowote !!

Ripoti za wizi kwenye ajali sio stori ngeni kwenye maeneo mengi ya nchi kama Tanzania, umewahi kuhisi kwamba hata Ulaya na Marekani hiyo kitu ipo?

Taarifa ikufikie kwamba imemkuta mama mmoja wa Kimarekani, Kimberly Smith ambaye alipata ajali na gari lake maeneo ya  Irving, Texas Marekani… gari ilipinduka mara tatu nje ya barabara

Mtu wa kwanza kufika eneo hilo alikuwa jamaa mmoja aliyesimamisha gari akajifanya kama anataka kutoa msaada kwa mama huyo kwa sababu alikuwa na majeraha na alikuwa amenasa ndani ya gari.

2CE0040E00000578-3252780-image-a-32_1443482860617

Badala ya kutoa msaada, huyo jamaa alimnyang’anya Kimberly pochi yake na kuingia kwenye gari yake, alafu akatokomea !! Baada ya muda kidogo akatokea msamalia mwingine ambaye alimsaidia mama huyo na kupiga simu ya dharura Polisi na Hospitali kwa ajili ya kumsaidia mama huyo.

2CE0041D00000578-3252780-image-a-11_1443481696941 2CE0041300000578-3252780-image-a-8_1443481654524 tumblr_inline_nve1ryjgFO1tvnn6i_500

Sasa mtu wangu kama ulidhani hii kitu inatokeaga huku pekeyake, kuwa macho.. watu wa aina hiyo wako kila sehemu !!

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments