Muziki wa Africa kwa sasa ni muziki unaosikilizwa na kufuatiliwa na watu wengi sana duniani tukiacha Waafrika wenyewe. Miezi kadhaa iliyopita tumeshuhudia wasanii kama Swizz Beats na Alicia Keys wakipost video zao kwenye Instagram wakiwa wanacheza ngoma za wasanii kutoka Africa kama Wizkid na Diamond Platnumz.
Leo nimekutana na tweets za rapper kutoka South Africa, AKA zinazowashambulia wale wote wanaomuuliza lini atafanya kazi na wasanii wa kimataifa, unajua jibu lake lilikuaje..? Kikubwa alichokigusia AKA kwenye tweets zake nne ni pamoja na kusema “kufanya collabo za kimataifa sio mpaka ufanye na wasanii wa nje ya Africa..!“
AKA amesisitiza kufanya collabo na wasanii kama Diamond Platnumz, Wizkid na Burnaboy wa Nigeria tayari ni collabo za kimataifa, na kama wewe ni mmoja ya wale wanaoamini kuvuka mipaka ni kuimba na msanii wa Marekani basi chukua hii kutoka kwa AKA kwenye hizi tweets zake nne hapa chini..
>>> “AKA lini utafanya wimbo na msanii wa KIMATAIFA? WTF Diamond, Wizkid, Burna na wengine ni LOCAL?! Update IOS yako tafadhali.” <<< @akaworlwide.
>>> “ mwisho wa siku ni suala la kujiamini na kuweka pembeni uoga. Binafsi NAJICHUKULIA KAMA MSANII WA KIMATAIFA. Unlock yourself“ <<< @akaworldwide
>>> “wanakufanya ufikirie INTERNATIONAL inamaanisha MAREKANI… Okamalumkoolkat & KO wapo Europe sasa hivi… HIYO INAKUAMBIA NINI KUHUSU AFRICA!?” <<< @akaworldwide.
>>> “watu wataichukulia hii kama ‘kupanic’ kwasababu ukweli huwa hauridhishi. Mnajidharau sana. AFRICA inabadilisha DUNIA..” <<< @akaworldwide.
Mpaka sasa AKA amesharekodi wimbo na Diamond Platnumz pamoja na kufanya feature kwenye single mpya ya Joh Makini ‘Don’t Bother’.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.