Habari za Mastaa

Tuko kwenye saa 48 za kujua mapya ya Alikiba, jingine ni hili la The Source Magazine

on

Tunaendelea kuyafahamu mambo 7 ambayo yanaendelea kutangazwa ndani ya saa 48 kumuhusu mwimbaji staa wa bongofleva Alikiba ambaye alikuja South Africa juzi May 18 na jana May 19 amesaini mkataba na kampuni maarufu ya muziki duniani iitwayo Sony Music.

Mkataba aliosaini Alikiba ni kama ule aliosaini Davido wa Nigeria, ni mkataba wa dunia nzima na sio Afrika kama baadhi ya Wasanii walivyosaini akiwemo Rose Muhando, na sasa moja kati ya yale mambo saba hili ni jingine… Alikiba ataandikwa kwenye toleo lijalo la jarida la Marekani maarufu kwa kuandika habari za mastaa wa muziki The Source Magazine.

Meneja wake aitwae Seven ameiambia millardayo.com >>> ‘Alikiba anakuwa msanii wa kwanza wa Tanzania kusaini mkataba na Sony World wide, ni mkataba wa miaka mitano, habari yake sio ndogo na sasa atatokea ameandikwa na Jarida maarufu la habari za mastaa Marekani The Source Magazine’

‘Atakua msanii wa kwanza wa Afrika Mashariki kuandikwa ndani ya hili jarida na hii itamsaidia kujulikana zaidi sababu ni jarida linaloaminika na linalosomwa na mamilioni ambapo kichwa cha habari kitasomeka kuanzia ukurasa wa mbele wa jarida hili’ – Seven
Sony 2

ULIKOSA KUONA ALIKIBA ALIVYOSAINI NA SONY SOUTH AFRICA? HAYA NI MAMBO MANNE KATI YA YOTE ATAYOYAPATA KWENYE MKATABA WAKE MPYA.

Soma na hizi

Tupia Comments