Michezo

Huenda ulipitwa na kile kilichowakuta Liverpool leo kutoka kwa Arsenal… hiki hapa

on

Wakiwa na majeruhi ya kipigo walichopata wiki mbili zilizopita kutoka kwa mahasimu wao Manchester United; Liverpool leo walisafiri mpaka jijini London kwenda kupambana na kuweka hai matumaini ya kuingia Top 4 kwa kucheza dhidi ya Arsenal.

Hata hivyo matumaini yao ya kuingia kwenye Top 4 yamezidi kupotea baada ya kukubali kupewa kibano cha magoli 4-1 kutoka kwa Arsenal.

Mpaka dakika 45 za kwanza zinamalizika ubao wa matokeo ulikuwa unasomeka Arsenal 3-0 Liverpool.. Hector Bellarin, Mesut Ozil na Alexis Sanchez wakiwa wafungaji wa magoli hayo.

Kipindi cha pili Liverpool walianza kwa kumuingiza Daniel Sturridge na kufanikiwa kupata goli moja baada ya Raheem Sterling kufanyiwa madhambi na Bellarin kisha Henderson akafunga mkwaju wa penati.

Huku dakika zikiwa zinayoyoma mwanasoka bora wa mwezi March katika EPL, Oliver Giroud alifunga goli zuri kabisa na kushindilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la Liverpool leo hii.

Kwa matokeo hayo Arsenal wamepanda mpaka nafasi ya pili kwenye ligi.

Msimamo wa Ligi ulivyo katika nafasi za juu Kaa karibu na millardayo.com nitakachokipata nitakusogezea hapa muda wowote kuanzia sasa, unaweza kujiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa >>>twitter Insta Facebook

Soma na hizi

Tupia Comments