Michezo

Zinazotajwa kuwa sababu za Arsenal kuwakosa Edinson Cavani, Karim Benzema na Lewandowski zipo hapa

on

Klabu ya soka ya Arsenal ilikuwa ikihusishwa kutaka kuwasajili wachezaji kadhaa katika dirisha la usajili lililofungwa mwezi August lakini haikufanikiwa na hatimaye ilifanikiwa kumsajili kipa wa zamani wa Chelsea Peter Cech kwa dau la pound milioni 10, miongoni mwa majina yaliyokuwa yakitajwa kutaka kusajiliwa na Arsenal ni Karim Benzema, Edinson Cavani na Robert Lewandowski.

hi-res-8c82e974577ebf25df8b128ad56dacb7_crop_north

Robert Lewandowski

September 24 stori kutoka mtandao wa express.co.uk umeandika chanzo cha Arsenal kuwakosa nyota hao, licha ya Robert Lewandowski kutopewa kipaumbele katika klabu yake ya FC Bayern Munich chini ya kocha Pep Guardiola, wakala wa mchezaji huyo Cezary Kucharski alithibitisha kuwa Lewandowski haipendi hali ya hewa ya Uingereza.

Karim-Benzema-celebrates--007

Karim Benzema

Karim Benzema alikuwa ni  mmoja kati ya mastaa wa soka waliokuwa wakisakwa na Arsenal katika kipindi cha usajili cha mwezi August, kwani alikuwa akihusishwa kujiunga na Arsenal kwa dau la poundi milioni 40. Lakini nguli wa zamani wa klabu ya Arsenal Ian Wright alilaumu mipango ya Arsenal kwani kilichofanya Arsenal wamkose Benzema ni kutokwenda kufanya mazungumzo ya awali na mchezaji kwani kufanya hivyo Ian Wright ana amini ingesaidia. Ila amekiri kuumizwa na tweet ya Benzema ya kusema Real Madrid ni nyumbani.

Paris Saint-Germain's Uruguayan forward Edinson Cavani celebrates after scoring a goal during the French League Cup round of sixteen football match between Paris Saint-Germain (PSG) and Saint-Etienne (ASSE) on December 18, 2013 at the Parc des Princes stadium in Paris. AFP PHOTO / THOMAS SAMSON (Photo credit should read THOMAS SAMSON/AFP/Getty Images)

Edinson Cavani

Kwa  upande wa Edinson Cavani licha ya picha ya yeye akiwa pamoja na kocha wa Arsenal Arsene Wenger kuvuja wakiwa Ufaransa, alinukuliwa kukiri kuhitajika na Wenger katika baadhi ya magazeti ya Ufaransa lakini amekuwa akiuhusishwa kujiunga na vilabu kadhaa katika dirisha la usajili la mwezi August lakini PSG ni mahali sahihi kwake na bado wanamuamini.

Wenger-352204

Wenger

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa, muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata,pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>YouTUBE

Tupia Comments