Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Joseph Kakunda amesema serikali imechukua hatua dhidi ya maduka binafsi ya kubadilishia fedha kwa sababu kulikuwa na ukiukwaji wa sheria.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kakunda amesema kuwa ipo sheria ya kusimamia biashara ya kubadilisha fedha ambapo mtu akienda maduka ya fedha lazima taarifa zake muhimu zichukuliwe ikiwemo kuangaliwa ‘Passport’.
“Hapa biashara ilikuwa holela ili kudhibiti biashara hiyo, mfumuko wa bei na thamani ya fedha yetu lazima tusimamie na hiyo biashara inayofanyika usiku ni kinyume na sheria,“amesema.