Mkongwe mwenye vyeo na heshima yake kwenye game ya Bongofleva, Ambwene Yessayah a.k.a AY karudi kuikamata chart ya muziki kwa mdundo wa ‘Zigo Remix‘ ambao umepitishwa kwenye mikono ya producers watatu wa Kitanzania.
Ujio huo wa January 2016 umekuwa mzuri kutokana na watu wengi kuipokea vizuri kwenye audio ya video yake, aliyepewa collabo hapo ndani ni Diamond Platmumz a.k.a Baba Tiffah… AY kamtaja staa wa Nigeria ambaye huenda angekaa kwenye collabo hiyo kama isingekuwa Diamond >>> ‘Ilikuwa nifanye na Wizkid… nikaona nifanye wimbo mwingine na Wizkid, kwa sasa nilihitaji tufanye na Diamond kuonesha tunaweza kushirikiana Watanzania wenyewe kwa wenyewe na muziki ukakamata vilevile‘- AY.
Sauti ya AY hii hapa kutoka kwenye story za 255 leo mtu wangu.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE