AyoTV

VIDEO: Mbunge ataka wanaume wanaobaka watoto wahasiwe

on

Headline za bunge la kumi na moja zimeendelea tena leo September 9 2016 ambapo katika kipindi cha maswali na majibu nakukutanisha na hii ya mbunge wa viti maalum CCM Najma Giga anayetaka serikali kuanzisha sheria ya kuwahasi wanaume wanaokutwa na kesi za ubakaji.

Je, serikali haioni haja ya kuweka adhabu tofauti ikiwemo kuwahasi wanaume wanaopatikana na tabia ya kuwaharibu na kuwabaka watoto‘ –Najma Giga

Naibu Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Hamis Kigwangalla ametolea majibu kwa kusema…>>>’Serikali inatunga sheria kwa kuzingatia katiba ya nchi na mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu, haitakuwa busara kuwahasi wanaume kwakuwa ni kinyume cha haki za binadamu

ULIMIS WAZIRI MKUU MAJALIWA VS FREEMAN MBOWE BUNGENI

Soma na hizi

Tupia Comments