Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Beyonce alipelekwa Mahakamani kwa madai ya kuiba wimbo… Mahakama imeamua haya!

on

Miezi michache iliyopita mmoja ya waimbaji kutoka kwenye bendi ya Beyonce Knowles, Javon Lane alipeleka mahakamani kesi ya haki miliki juu ya wimbo wa XO wa Beyonce na kudai kuwa msanii huyo alimuibia wimbo wake alioupa jina XOXO kisha akaubadilisha na kuuita XO baada ya kumuomba asikilize demo yake na kugundua kuwa wimbo ni hit song… Leo mambo yapoje?

BEE3

Beyonce Knowles.

Wiki iliyopita tarehe 21 October 2015, Beyonce Knowles alishinda kesi ya haki miliki juu ya wimbo huo baada ya Mahakama ya New York kutupilia mbali madai ya Javon. Lakini mwimbaji wa Beyonce, Javon amesema hajakubaliana na uamuzi wa Mahakama ya New York na anategemea kukata rufaa.

Mwanasheria wa Javon Lane, Domenick Nati amesema kuwa mteja wake amesikitishwa na uamuzi wa Jaji wa Mahakama hiyo ila kwa sasa yeye na mteja wake wanapanga mipango ya kukata rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama hiyo.

BEE2

Jovan Lane pia ni backup singer kwenye bendi ya Beyonce.

Kwa mujibu wa Jaji Paul Engelmayer, kuna tofauti kubwa sana kati ya wimbo wa Beyonce wa XO, na wimbo wa Javon Lane XOXO, jaji huyo amesema kuwa mashairi ya wimbo wa XOXO yamekaa ‘kimapenzi’ zaidi wakati wimbo wa XO wa Beyonce umebeba ‘ujumbe wa maisha na upendo kwa ujumla’, hivyo hoja ya Javon haina mashiko kwenye kesi hiyo.

Nimekusogezea nyimbo zote mbili hapa chini, unaweza ukazicheki kujua kama zina utofauti au kama zimefanana.

  1. Beyonce – XO.

2. Javon – XOXO.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments