Ishu ya mashambulizi ambayo yametokea Afrika Kusini imechukua HEADLINES kwa zaidi ya wiki moja.. labda hakuna aliyetegemea hali hii kujirudia, sio mara ya kwanza kuona wageni wakishambuliwa Afrika Kusini.. Picha na Video ziko nyingi Whatsapp zinaonesha watu wanauawa, wengine wanaumizwa.
Hizi ni Tweets sita za Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ameandika kuhusu hali inayoendelea Afrika Kusini.
Right! I will hold a press conference at 11am this morning on the subject and steps ahead… https://t.co/WLZglO79lF
— Bernard Membe (@BernardMembe) April 20, 2015
Tanzania imesikitishwa na inalaani vikali vitendo visivyo na ubinadamu vya vurugu na mauaji ya wageni na mali zao huko Afrika Kusini (1/6).
— Bernard Membe (@BernardMembe) April 20, 2015
Kama Waziri-Nje,nimeongea na Waziri wa Usalama wa Afrika Kusini na nimemuita Balozi wake hapa nchini kueleza masikitiko yetu (2/6)
— Bernard Membe (@BernardMembe) April 20, 2015
Hakuna Mtanzania akiyepoteza maisha kutokana na Xenophobia.Vifo vya Watanzania 3 vilivyoripotiwa ni kutokana na sababu nyingine tofauti(3/6)
— Bernard Membe (@BernardMembe) April 20, 2015
Tuna Watanzania 23 katika kambi ya Isipingo,Durban ambapo zaidi ya watu 3000 kutoka nchi mbalimbali wapo.Kati yao 21,wako tayari kurudi(4/6)
— Bernard Membe (@BernardMembe) April 20, 2015
Tunashirikiana kwa karibu na Serikali ya Afrika Kusini kuhakikisha Usalama wa Watanzania na pia wanaostahili kurudi wanarejeshwa (5/6)
— Bernard Membe (@BernardMembe) April 20, 2015
Tunapongeza Serikali ya Afrika Kusini kwa kuchukua hatua za haraka na pia tamko la M/Kiti wa SADC dhidi ya mauaji haya.Sisi ni ndugu! (6/6)
— Bernard Membe (@BernardMembe) April 20, 2015
Mwamvita Makamba ni Mtanzania mwenzetu anayeishi Afrika Kusini, alifanya exclusive interview na millardayo.com, akasema yeye pia alijikuta katikati ya kundi la vijana ambao walikuwa wamechoma matairi barabarani, wakalizunguka gari na kutaka kumshambulia, alifanikiwa kutoka salama.. lakini hii ishu haikuhusiana na vurugu za ubaguzi wanazofanyiwa wengine.