Kwa mujibu wa mtandao TMZ umeripoti kuwa kundi la muigizaji wa tamthiliya ya Empire Jussie Smollet linasikitika na taarifa ambazo zilitokea mapema mwezi January na watu kudhani kuwa ni taarifa za uwongo kuhusiana na ishu ya ubaguzi wa rangi na jinsia aliofanyiwa Jussie mjini Chicago.
Inaelezwa kuwa Jussie Smollet aliongea na mmoja wa rafiki zake ambaye anafahamika kwa jina la Abel Osundairo siku nne kabla ya tukio hilo kutokea na alimuomba waonane huku akisisitiza kuwa anahitaji msaada wa kuongea nae uso kwa uso na sio kwa simu, hata hivyo Jussie Smollet alikana meseji hizo kuhusika na tukio alilofanyiwa na kudai kuwa alitaka kumuagiza dawa za kupunguza mafuta ambazo zinapatikana Nigeria na haziruhusiwi kuingia nchini Marekani.
Inaelezwa kuwa kundi hilo limekasirika kutokana na Polisi kudhani kuwa Abel na Jussie waliusuka mpango mzima wa tukio la uvamizi ili lionekane ni kweli hii ni baada ya kuonekana kwamba Jussie alimpigia simu rafiki yake Abel. Taarifa zinadai kuwa Jussie alimpigia Abel kumjuza kuhusu ratiba ya mazoezi na si vinginevyo.
Hata hivyo imeelezwa kuwa uvamizi uliofanyika dhidi ya Jussie ni kweli na kesi kwa sasa bado ipo mikononi mwa Polisi na kundi hilo linasikitika na vyombo vya habari kuripoti kuwa waliomfanyia ubaguzi Jussie ni watu wenye asili ya wazungu.
VIDEO: MUZIKI WA ALIKIBA UMEMFIKIA KAMANDA WA POLISI KAGERA