Mchezaji wa zamani wa mpira wa kikapu NBA Lamar Odom’39 ambaye pia alijipatia umaarufu mkubwa baada ya kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na Khloe Kardashian ameweka wazi kuwa anajuta kutofata ushauri ambayo aliwahi kupewa na Rapper Jay Z.
Kupitia mahojiano aliyoyafanya na ‘Peolpe’s Party With Talib Kweli” Lamar alifunguka na kusema Jay Z alimpa ushauri kuhusu muziki wa Hip Hop pale alipojaribu kuingia kwenye muziki na alipofungua Record Label yake ya ‘Rich Soil’ na alimwambia afanye kitu kingine tofauti na hicho lakini alihisi kuwa Jay Z alikua akimuonea wivu.
“Nakumbuka nilivyokutana na Jay Z nadhani alikuwa akipokea tuzo na aliniambia wewe unafanya nini na huu muziki wa Rap? nikamwambia nina msanii ambaye nilimuamini na bado namuamini anaitwa Ali Vegas na alisema hapana mshikaji unatakiwa kuwekeza kwenye makazi” >>> alisema Lamar
Lamar alifunguka na kuweka wazi anatamani angesikiliza ushauri aliopewa na Jay Z au huenda kipindi kile Jay Z aliogopa ushindani ambao ungekuwepo kwenye industry nzima ya muziki ya Hip Hop.
VIDEO: ALIKIBA KAZUNGUMZA SABABU ZA GARI LAKE KUTOKUENDESHWA NA MTU MWINGINE “SIPENDI”