Mix

Afisa Mtendaji anaedai kushambuliwa na wafuasi wa Chadema

By

on

SONY DSCMwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Khamis M. Mgeja alikwenda kumpa pole Afisa Mtendaji wa kata ya Ubagwe katika halmashauri ya wilaya ya Ushetu Alphonce John Kimario aliyejeruhiwa kwa kushambuliwa na mapanga na watu aliowataja kuwa ni wafuasi wa Chadema.

SONY DSCHii inasemekana kutokana na vurugu zilizotokea jioni ya February 04,majira yakiwa ni saa 1 usiku katika kata ya Ubagwe muda mfupi baada ya kumalizika kwa kampeni za kumnadi mgombea wao.

SONY DSCAkizungumza na waandishi wa habari Afisa huyo Mtendaji wa kata ya Ubagwe Alphonce John Kimario amesimulia kuwa pamoja na kuumia vibaya machoni hasa jicho lake la kulia pia analalamika juu ya maumivu makali.

Maumivu anayodai kuyasikia kwa sasa Kimario yapo sehemu za mgongoni na hii ni mara baada ya kupigwa na nondo ambapo kwa hivi sasa upande wa kulia pamoja na bega lake umekufa ganzi Kimario ambaye amepigwa nondo,mapanga na kwenye paji la uso kiasi cha kushonwa nyuzi kadhaa na kutobolewa jicho moja kwa sasa amekimbizwa hospitali ya Rufaa Bugando kutokana na hali yake kuwa mbaya zaidi.
Majeruhi wengine  kama Masoud Melimeli (katibu Mwenezi wa Wilaya) amebaki katika uangalizi wa Hospitali ya Wilaya akiwa na majeruhi wengine kama Ramadhani Salum (Umoja wa Vijana) na Mussa Daudi (Katibu Uchumi Kata ya Nyihogo) ambaye alilazwa katika Hospitali ya wilaya ya Kahama na mara baada ya kuzidiwa amepakiwa kwenye Ambulance na kuwahishwa Bugando kwa ajili ya matibabu zaidi.

Tupia Comments