Habari za Mastaa

Hivi ndivyo Tht walivyokuwa wakishoot Dvd yao na kuwatambulisha waimbaji wapya

By

on

5Usiku wa February 06 umekua ni usiku uliopambwa na sauti mbalimbali za waimbaji toka Tht ambao wamekaa jukwaani zaidi ya masaa 3 wakirekodi Dvd yao huku wakitoa burudani kwa waalikwa waliopata mualiko huu ambapo shughuli hiyo imeenda sambamba na kuwatambulisha waimbaji wapya kutoka band hiyo.

2Wasanii wapya waliotambulishwa kama waimbaji wapya toka band ya Tht ni Lulu,Husein,Alice aliyeshirikishwa na Ben pol kwenye wimbo wa pete na Khadja mwenye wimbo wa Maumivu ulio kwenye chart za juu redio mbalimbali Tanzania kwa sasa.

10Nafasi hii pia ilitumiwa kuwakumbusha waimbaji mbalimbali waliowahi kuwa Tht kipindi cha nyuma ambapo On stage Marlow aliimba pamoja na wana Tht wote akiwemo Barnaba,Ditto,Amini,Linah,Mataluma na Mwasiti.

Baadhi ya wasanii waliohudhuria kwenye party hii iliyopewa jina la Acoustic Musical Concert ni pamoja Linex,Queen Darlin,Fid Q,Joh Makini na wengine wengi waliopata mualiko huu uliofanyika pembeni ya fukwe za bahari ya hindi pale Escape 1.

Pichaz zinafuata baadae kidogo endelea kuwa karibu na familia ya millardayo kupitia Instagram.com, facebook.com, twitter.com/millardayo pamoja na kutembelea hapa www.millardayo.com.

Tupia Comments