Mix

CHADEMA mchana huu baada ya jina “Mbowe” kutajwa kwenye orodha ya Makonda

on

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda leo February 8 2017 ametangaza kuiachia orodha ya Watu 65 wanaotuhumiwa kwa biashara ya dawa za kulevya ambapo amemtaja pia Mbowe ndani yake.

Dakika chache baada ya kumtaja, CHADEMA Makao makuu Dar es salaam walikutana na Waandishi wa habari na kusema yafuatayo >>> “Kimsingi katika majina mengi yaliyotajwa kuna jina la Mwenyekiti wa chama Mbowe, swala la utetezi wake au maelezo hilo ni swala binafsi sababu kilichotajwa ni jinai lakini kimsingi tunachukua nafasi hii kulaani

Tunalaani jinsi tusivyoweza kuendesha utawala wa sheria kwenye nchi yetu na jinsi tusivyofata kanuni zilizowekwa dhidi ya sheria, Mh. Mbowe ni kiongozi wa kitaifa, ni kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, ni Mbunge wa Hai…. kwahiyo kuna taratibu za kufata unapokua na kusudio la kumuita

Kitendo cha kwenda kuongea kwenye mkutano na Waandishi wa habari na kutaja viongozi wakuu wa kitaifa ambao wana tuhuma tu ambazo hazijathibitishwa, ni kukosa ustaarabu wa kiuongozi… tusingependa kuona viongozi wengine Waandamizi kutendewa kama alivyotendewa kiongozi wa chama chetu” 

Mtazame zaidi kwenye hii video hapa chini

Soma na hizi

Tupia Comments