Michezo

Challenge ya muamuzi wa Tanzania yafika hadi UK

on

Wakati huu wa mlipuko wa virusi vya corona uliyopelekea kusimama kwa shughuli mbalimbali duniani, kwa upande wa michezo watu wengi wameandaa challenge za kujifariji.

Tumeona wachezaji mbalimbali wakibuni challenge na kupokelea vizuri ila muamuzi wa kitanzania Frank Komba alikuwa muamuzi wa kwanza kubuni challenge yake ambayo imefika sehemu mbalimbali duniani.

Komba alivaa sare za waamuzi akiwa nyumbani kwake na kuamua kufanya kama linesman (mshika kibendera) akichzesha mpira, challenge ambayo imefika sehemu mbalimbali ikiwemo ukurasa rasmi wa shirikisho la soka Afrika CAF na sasa mtandao wa dailymail.co.uk umeandika habari hizo.

 

Soma na hizi

Tupia Comments