Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi mweka hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo, Thomas Chogolo ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili za ubadhilifu wa makusanyo ya mapato ya Halmashauri hiyo.
Laakini pia amewataka Watendaji wa Halmashauri huyo kumaliza haraka migogoro yao ya kiutendaji kabla ya Serikali haijawachukulia hatua kwani wanachokifanya ni kinyume na maelekezo yake.
Waziri Mkuu amechukua hatua hiyo wakati akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Kigoma.
“WANANIFANYIA HILA, HAKIKA HAWATANITOA”-MKURUGENZI DODOMA