Habari za Mastaa

“Nashindwa kuelewa kama walinituhumu kweli nimeiba cheche” – Dimpoz

on

Mwimbaji wa Bongofleva Ommy Dimpoz alikaa kwenye On Air with Millard Ayo na kuzungumza ishu mbalimbali baada ya kusaini kuwa chini ya management ya Rock Star ikiwemo ishu ya kutuhumiwa kuiba wimbo wa cheche.

Dimpoz alisema “Kwanza nashindwa kuelewa, sikupata statement sahihi kutoka upande wa kina Abby Dadi lakini kama wameongea hivyo watakua wamekosea… siku naitambulisha hii ngoma kwenye XXL nilisema sikuiandika mimi, iliandikwa na Lolly Pop na kuwa produced na Kid Boy (Dope tunes).

“Dope Tunes ndio wenye credits na nilishamalizana nao kuwalipa kila kitu, ngoma ilipotoka ndio nimepata comments za watu kwamba sio wimbo wangu ikabidi niwaulize Dope Tunes wakasema hata sisi tunashangaa sababu Lolly Pop anasema wakati anatengeneza hiyo idea aliianzia kwenye studio ya Abby Dadi’

Full Interview Ommy Dimpoz akiongea bonyeza play hapa chini

VIDEO: “Mimi na Wema Sepetu tunakutana sana” – Diamond Platnumz…… Full Video hapa chini

Soma na hizi

Tupia Comments