Siku 11 baada ya klabu ya Dar es Salaam Young Africans kucheza mchezo wake wa kwanza wa hatua ya mtoano ya 16 ya Kombe la shirikisho barani Afrika CAF, Leo May 18 2016 Yanga waliifuata GD Esperanca ya Angola kucheza mchezo wa marudiano, katika mchezo huo Yanga imekubali kipigo cha goli 1-0.
Goli ambalo lilifungwa na Kabungula dakika ya 25, kwa matokeo hayo Yanga wanafanikiwa kutinga hatua ya Makundi ya Kombe la shirikisho barani baada ya kuitoa Esperanca kwa jumla ya goli 2-1, hiyo inatokana na Yanga kuifunga Esperanca goli 2-0 katika mchezo wa kwanza uliochezwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
#MillardAyoUPDATES #FullTime GD ESPERANCA 1(#KABUNGULA 25′) -0 YANGA (AGG 1-2) #CAF pic.twitter.com/TUFPvJCp4s
— millard ayo (@millardayo) May 18, 2016
ALL GOALS: YANGA VS GD ESPERANCA MAY 7 2016, FULL TIME 2-0
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE