Habari za Mastaa

Bidhaa za Fenty zamuweka kwenye rekodi Rihanna na kampuni ya LVHM

on

Leo May 10,2019 kampuni kubwa na maarufu ya bidhaa za kifahari ya LVMH ya nchini Ufaransa imemtangaza mwimbaji Rihanna kama mshirika wao mpya kibiashara ambapo atatengeneza bidhaa zenye Brand yake kupitia kampuni hiyo.

LVHM inahusika kutengeneza na kusambaza bidhaa kama Mvinyo, Mavazi ya Ngozi ya Brand kubwa kama Louis Vuitton na Fend pia Saa za Mkononi na Manukato. Kampuni hiyo ikiwa na miaka 32 inamtaja Rihanna kuwa mwanamke wa kwanza kupata ushirika na Kamapuni hiyo ya LVHM kupitia bidhaa zake za Fenty kuwa za kwanza kuingia kufanya kazi na LVMH tokea mwaka 1987  zilipowahi kuungana na Christian Lacroix.

“Ni siku kubwa kwa utamaduni asante Mr. Arnault kwa kumuamini binti mdogo kutokea kwenye kisiswa na kunipa nafasi ya kukua na wewe kwenye LVMH, hiki ni kithibitisho kuwa hakuna kitu kisichowezekana, Neema kwa Mungu” >>> aliandika Rihanna.

Inaelezwa pia Rihanna amekuwa kimya kwenye kazi zake za kimuziki kwa miaka mitatu na amejikita zaidi kwenye kutengeneza bidhaa zake za urembo zenye Brand yake ya ‘FENTY BEAUTY’ ambazo zinafanya vizuri kwa sasa ndani na nje ya Marekani.

VIDEO: WAGANDA WAGEUZA MSIBA WA DR. MENGI FURSA, JAMAA WAMEPIGA HELA

Soma na hizi

Tupia Comments