Habari za Mastaa

Rapper Offset anusurika na risasi zilizopigwa nje ya studio (+video)

on

Inaripotiwa kuwa watu wasiojulikana wameonekana wakijaribu kufanya shambulio la kupiga risasi kwenye studio ambayo inasemekana alikuwepo rapper kutokea kwenye kundi la Migos, Offset mwenyewe alikuwa ndani ya studio akirekodi.

Inaelezwa mpaka sasa bado haijajulikana sababau iliyowafanya washambuliaji hao kufanya tukio kama hilo na tayari Polisi mjini Atlanta wanaendelea kufanya uchunguzi ili kuwabaini wahusika. Inaripotiwa kuwa hakuna mtu ambaye amejeruhiwa mpaka sasa.

Inaelezwa kuwa watu hao walivamia eneo hilo saa tatu usiku siku ya Jumatano May 8,2019 na kuripotiwa kuwa risasi ziliharibu mlango pamoja na magari matatu yaliokuwa eneo hilo na mashuhuda wakidai kuwa mlengwa wa tukio hilo alikuwa ni Offset japo hawakufanikiwa.

VIDEO: Ulipitwa na hii ya msanii Ommy Dimpoz kujiuliza “Ni mimi kweli?”, RIP Dr. Mengi, Bonyeza PLAY hapa chini kutazama 

Soma na hizi

Tupia Comments