April 18, 2017 zilizagaa taarifa kuwa kuna mwanamke mkazi wa Tanki Bovu jijini Dar es Salaam kufariki baada ya kugongwa na gari usiku wa Sikukuu ya Pasaka, lakini alikutwa makaburini akiwa hai licha ya ndugu zake kuthibitisha amekufa.
Kupitia Heka heka ya Clouds FM leo April 19, 2017 mtangazaji Geah Habibu ametuletea undani wa stori hiyo ambayo inamuhusu mwanamke anayefahamika kwa jina la Anna ambaye inadaiwa aligongwa na gari ikathibitika kuwa amekufa lakini yakatokea mengine ya kustaajabisha baada ya kudaiwa hakufa bali aliyekufa ni jirani ambaye aligongwa na gari wakati anavuka barabara huku Anna akidaiwa kuchukuliwa kimazingara.
Bonyeza Play hapa chini kusikiliza Full story...
VIDEO: Maajabu mengine ya jiji la Dar, mwanamke adaiwa kufa kisha kufufuka..