Mwanaume mmoja nchini Nigeria anayefahamika kwa jina la Chidimma Amedu ameshangaza watu siku chache zilizopita baada ya kupata mchumba na kumuoa ndani ya siku sita baada ya kuandika kwenye ukurasa wake kuwa anatafuta mwanamke wa kumuoa.
Katika akaunti yake hiyo Chidimma aliandika kuwa anatafuta mke wa kuoa na kwa binti yeyote atakayetaka kuolewa naye aandike pale na yeye atafatilia maombi hayo na kuchagua atakayekuwa amevutiwa naye zaidi na kuongeza kwamba atamuoa January 6, 2018.
Wengi wali-comment na moja kati mabinti hao Sophy Ijeoma anasema aliandika kwa utani kuwa naye angependa kuolewa naye hivyo amtumie message. Chidimma alipopitia maombi yale akavutiwa zaidi na Sophy na akampigia voice call Facebook na wakazungumza kwa mara ya kwanza.
Kwa mujibu wa wawili hao walipozungumza na BBC walisema Chidimma baada ya siku mbili alisafiri kutoka Abuja alipokuwa akiishi kwa kilometa 500 kumfuata Sophy katika mji wa Enugu na walipoonana walipendana na taratibu zote za ndoa zikafanywa kwani katika kijiji hicho hicho walikuwepo pia ndugu wa Chidimma.
Alipofikia Mrema kuhusu aliyemzushia kifo “nitadai bilioni 20 haitapungua hata thumni”
‘Gumzo Mtwara wananchi wakesha wakinywa uji, Wakiofia kufa kwa utabiri