Michezo

Mashabiki wanaoaminika kuwa wa Yanga waichanachana jezi ya Simba, Manara kafunguka

on

Afisa habari wa Simba SC Haji Manara ametumia ukurasa wake rasmi wa instagram kueleza masikitiko yake, baada ya kupost clip video inayoonesha watu wanaodhaniwa kuwa mashabiki wa Yanga wakiichanachana jezi ya Simba SC ya msimu huu mpya wa 2019/20, Manara ameandika haya kwenye ukurasa wake wa instagram.

“Nawasihi sana Washabiki wote wa Soka nchini tusifanye hv vitendo vya hovyo hovyo Kwenye mchezo huu murua nchini na kote duniani!! haikubaliki na inaweza kusababisha mabaya kwa soka letu,Yanga na Simba ni watani wa jadi na wapinzani wa uwanjani,sio maadui wala mahasimu”

“Sote tukemee mambo ya kishamba na kwa Washabiki wa simba nawaomba msithubutu kuchana Jezi ya watani zetu,tuishie kucharurana na kutaniana ,hii ndio misingi tuliyoirithi toka kwa Waasisi wa hv vilabu!!”

VIDEO: MWALIMU KASHASHA KATOA TATHMINI KWA YANGA HII DHIDI YA TOWNSHIP ROLLERS

Soma na hizi

Tupia Comments