Premier Bet
TMDA Ad

Mix

Kilichowakuta Mchungaji na waumini wake kwenye ibada ya mazishi makaburini..

on

image130Mhubiri mmoja huko Brazil, Alex Novais de Brito aliyekuwa akifanya mahubiri kwenye mazishi ya muumini wake amejikuta akishindwa kumaliza ibada hiyo baada ya udongo wa kaburi kudidimia na kufanya Mchungaji huyo na waumini wengine watatu kudumbukia kwenye kaburi.

Hilo lilitokea kwenye makaburi ya Campo da Esperanca wakati kukifanyika ibada ya mazishi.

Watu wawili walipelekwa Hospitali ya jirani ili kutibiwa majeraha madogo waliyoyapata baada ya kuanguka, watu walichanganyikiwa baada ya kutokea tukio hilo, Mhubiri huyo alijikuta kwenye wakati mgumu na kushindwa kumalizia ibada.

Hakuna Stori itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Tupia Comments