Kama umefatilia vizuri mitandao ya kijamii siku za hivi karibuni, basi huenda ukawa umekutana na sauti ya mama Wema akidai kuwa kuna marafiki wanamfundisha tabia mbaya mwanae huku akitaja jina la mwigizaji Diana na kumuomba akae mbali na mwanae kwani anampoteza.
Maneno mengi yamekuwa yakiendelea kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo sauti hiyo inayosambaa ikidaiwa kuwa ya mama Wema huku kila mtu akitoa mawazo yake kuhusiana na maneno aliyoyaongea mama wema, huku akiwataka na team Wema kuachana na mwanae.
Kupitia ukurasa wa instagram wa Wema Sepetu ameamua kuzima ishu hiyo na kumshukuru mama yake kwa kuendelea kuwa naye kwenye maisha yake.
“After all is said and done, I will forever be grateful to have you in my life ❤” >>>Wema Sepetu
ULIPITWA NA VANESSA MDEE KUILETA ALBUM YA PILI, PRODUCER WA BEYONCE KAHUSIKA? BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA.