Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

Game ya Simba SC vs JKT Tanzania imeahirishwa Jamhuri Morogoro

on

Leo Jumatano ya April 3 2019 ulikuwa uchezwe mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2018/2019 kati ya Simba SC dhidi ya JKT Tanzania katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, mchezo huo ulikuwa ni wakiporo.

Kutoka uwanja wa Jamhuri Morogoro ulipokuwa uchezwe mchezo huo wa Simba SC dhidi ya JKT Tanzania kujaa maji, basi mchezo huo umeahirishwa na utapangwa siku nyingine hauwezi kuchezwa siku inayofuata kama sheria inavyosema lakini utapangwa tarehe nyingine.

Huo ulikuwa ni mchezo wa kiporo wa Simba SC akiwa anaimalizia kati ya michezo yake 6 ya viporo, Simba haiwezi kucheza mchezo huo siku inayofuatia kwa sababu ina mchezo wa robo fainali ya CAF Champions League dhidi ya TP Mazembe hivyo sheria inasema timu inatakiwa ipumzike saa 48 kabla ya kucheza mchezo mwingine tena.

Msimamo wa Samatta kuhusu hatma ya Kapombe katika mgao wa Taifa Stars

Soma na hizi

Tupia Comments