Michezo

PICHA: Simba SC kisichoriziki hakiliki kwa Sevilla FC

on

Club ya Simba SC leo ilipata nafasi ya kipekee kupambana na moja kati ya timu mahiri za Ligi Kuu Hispania LaLiga club ya Sevilla FC ambao ni Mabingwa mara tano wa Europa League katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Simba SC ambao ni wenyeji unaweza kusema kisichoriziki hakiliki kutokana na kuongoza kwa magoli 4-2 lakini dakika za mwishoni kabisa Sevilla wakapindua matokeo kwa kufunga magoli 5-4, hatimae mchezo ukamalizika kwa Simba kushindwa kuwaondoa mashabiki wao wakiwa na nyuso za furaha.

Hii ndio mara ya kwanza kwa timu ya kwanza ya LaLiga kuja Tanzania kucheza mchezo wa kirafiki kitu ambacho kimeleta hamasa kwa wachezaji vijana, kupata nafasi ya kumuona mchezaji kama Jesus Navas aliyewahi kuichezea FC Barcelona ya Hispania.

 

 

 

Mapokezi ya Sevilla Tanzania waliokuja kukipiga na Simba SC

Soma na hizi

Tupia Comments