Habari za Mastaa

Burna Boy kuidondosha Album ya nne ‘African Giant’

on

Mshindi wa tuzo ya Best International Act kwenye BET mwaka 2019 Burna Boy ametangaza tarehe rasmi ya kuidondosha Album yake ya ‘African Giant’ ambapo amesema kuwa Album hiyo  itaachiwa rasmi July 26,2019.

Burna Boy ametangaza ujio wa album yake hiyo mpya “African Giant” kupitia ukurasa wake wa twitter ambapo pia ametuonyesha cover ya Album ikiwa imeelezwa kuwa African Giant itabeba jumla ya ngoma 16 ikiwa tayari ngoma nne ameshaziachia ikiwemo On The Low, Dangote, Gbona na Anybody.

Album hiyo itakua ni ya nne ambapo album yake yake ya tatu ‘Outside” aliiachia January 26, 2018 ikiwa album hiyo ilijuisha midundo ya Afro Pop, Rap pamoja na dancehall ilihusisha sauti za wakali kutokea Uingereza kama J Hus, Lilly Allen and Mabel

VIDEO: AUNT EZEKIEL, SHILOLE, SHAMSA FORD, WAFUNGUKA KUHUSU SWAHILIFLIX MTANDAO UTAKAOUZA KAZI ZAO

Soma na hizi

Tupia Comments