Msanii wa Bongofleva Mwana FA ambaye pia ni mshabiki mkubwa wa Man United Mwana FA leo amepata bahati ya kukutana na kocha wa zamani wa Man United Jose Mourinho ambaye alifutwa kazi December 2018, Mwana FA alikuwa ni sehemu ya mashabiki wa Man United waliokuwa wanatamani Mourinho afutwe kazi.
“mara paaap,chuma hiki hapa..nikifute kazi tena?😂..no man natania ,nilifurahi kukutana na Jose Mourinho leo..yale maneno mabaya yote nikayaficha,nikamshukuru kwa nyakati nzuri alipokuwa kwetu na kumtakia bahati njema popote anapokwenda..na kuwa mimi ni mshabiki wake mkubwa,hasa anapoanza kuchonga..i feel good kukutana na this great man!”>>>Mwana FA
Man United wiki hii itakuwa na kazi ngumu ya kucheza mchezo wa pili wa marudiano wa UEFA Champions League dhidi ya FC Barcelona katika uwanja wa Nou Camp, Man United wakiwa wanataka kufuzu chini ya Ole Gunnar Solskjaer watahitaji ushindi wa 2-0 na kuendelea ili wafuzu kucheza hatua ya nusu fainali baada ya game ya kwanza kupoteza 1-0.
Kutokea Algeria, Morocco na Hispania Ulimwengu, Msuva na Chilunda kuhusu Kundi C AFCON 2019