Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Halle Berry na mume wake kuachana baada ya miaka miwili ya ndoa!? Ukweli huu hapa…

on

Muigizaji wa movie Hollywood, Halle Berry anaziandika headlines za leo kwenye kurasa za burudani baada ya yeye na mume wake kuweka wazi kuwa wanaachana baada ya kushindwa kurekebisha tofauti zao kama wanandoa!

halle2

Halle Berry na mume wake Olivier Martinez.

Halle Berry na mume wake Olivier Martinez walifunga ndoa kubwa mwaka 2013 na pamoja walifanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume, Maceo lakini leo kutokana na tofauti ambazo zimeshindwa kutatuliwa, wawili hao wameamua kuweka hali yao wazi na kuuambia mtandao wa ET kuwa wameamua kupeana talaka.

Berry na mume wake Martinez walipeleka Mahakamani ombi lao la talaka siku tarehe 26 October na kuiridhisha Mahakama kuwa wameshindwa kutatua tofauti zao kama wanandoa hivyo wangependa kama Mahakama imekubali ombi lao pamoja na kupewa haki sawa za kumtunza mtoto wao wa kiume mwenye miaka miwili.

halle3

Halle Berry na mtoto wake wa kiume, Maceo.

Kwa mujibu wa documents zilizowekwa wazi kwa mtandao wa ET wawili hao waliamua kutengana rasmi tarehe 26 October na kisha kufungua maombi ya talaka Mahakamani. Kwenye document hizo, wawili hao walisema..

>>> ” Mioyo yetu ni mizito kwani hatukutegemea kuwa mambo yangefika huku, tumeamua kufanya hivi na kusonga mbele kwa amani na kwa heshima ya kila mmoja alionayo juu ya mwenzake na pia kwa kufocus kwa kile ambacho ni bora zaidi kwa mtoto wetu na sio kile kilicho bora zaidi kwetu sisi wazazi. Tunakatiana kila la lheri kwenye maisha, tunaombeana maisha mema yenye amani na upendo. Lakini pia tunatumaini kuwa mitandao na websites itaheshimu maamuzi yetu na pia kuheshimu zaidi privacy ya maisha yetu na ya mtoto wetu kwenye kipindi hiki kigumu…” <<< nukuu kutoka mtandao wa ET.

halle4

Halle Berry na mtoto wake wa kike Nahla.

Hii itakuwa ndoa ya tatu ya Halle Berry kuvunjika, hapo awali alikuwa mke wa mchezaji wa baseball David Justice lakini kabla ya ndoa yake na mchezaji huyo Halle alikuwa mke wa mwimbaji Eric Benet.Ukiacha hayo, Halle Berry alishwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na model Gabriel Aubry ambaye alifanikiwa kupata nae mtoto mmoja wa kike, Nahla mwenye miaka 7 sasa hivi.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments