Kwenye Hekaheka ya leo kuna tukio la mauaji la kijana mmoja limetokea nyumbani kwa mama wa mke wake ambalo limeleta utata,
Tukio limetokea Mwembechai, Dar es salaam ambapo awali inasemekana kuwa alipotea katika mazingira ya kutatanisha.
Mjomba wa marehemu amezungumza kwenye Hekaheka na kusema alifikiwa na taarifa akiwa kazini kwake Kariakoo..akaamua kutoka na kwenda eneo la tukio.
Anasema walipewa taarifa kuwa ndugu yao huyo alipotea na wakaamua kumtafuta bila mafanikio ndipo walipoamua kwenda katika hospitali mbalimbali na walipomkosa wakatoa taarifa kituo cha Polisi lakini mke wa marehemu alikua hataki waende kutoa taarifa kituo cha Polisi Magomeni.
Mke katoa maelezo Polisi na kusema kuwa kuna jamaa alimpigia mume wake wakafanye biashara..baada ya muda jamaa akarudi na kumtafuta marehemu lakini hakuweza kumpata, mke aliamua kwenda nyumbani kwa mama yake na alikuta sandals za mume wake nje, alipomuuliza mama yake akaambiwa ameondoka na rafiki zake.
Msikilize hapa Mjomba wa marehemu akizungumza na Geah Habib..
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM,