Leo ni mwendeleo wa hekaheka ya jana ambayo ilihusu jirani mmoja huko Kivule, Dar es salaam kudaiwa kuwanyanyasa majirani wenzake hadi kuwafikisha kituo cha Polisi.
Jana kulikuwa na kikao cha wanakijiji wote na viongozi wa kijiji..baada ya ya wananchi kutoa malalamiko yao, muhusika anayetuhumiwa amesema hayo yote anayoshutumiwa si kweli bali anasingiziwa.
Kikao hakikuweza kufikia muafaka wakati wakijadili suala la nguzo za umeme kupita katika eneo la viwanja vyake, kulitokea majibizano na hawakuweza kuelewana, hivyo kuvunjika kwa kikao hicho.
Anayelalamikiwa anasema majirani zake hawakumuomba kupitisha nguzo..kuhusu eneo la msitu amesema hakuna msitu ni miti tu amepanda ambayo inamsaidia kumpa kivuli pamoja na kulisha mifugo yake
Amesisitiza nguzo za umeme zilizowekwa kwenye kiwanja chake zitolewe na ziwekwe kwenye maeneo yao kama watashindwa kulipa gharama za kuweka ambazo alitaka alipwe milioni 2.
Wasikilize hapa wananchi wa Kivule wakizungumza na Geah Habib..
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE