Millard AyoMillard Ayo
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
  • Contact
Search
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Reading: BREAKING: Mahakama ya Kisutu imemuachia huru Askofu Gwajima
Share
Notification Show More
Latest News
Jorginho aondoka Chelsea na kusaini Arsenal
February 1, 2023
Rais Samia ashtukia mchezo mchafu hela za Plea Bargain
January 31, 2023
Rais Samia ainyooshea kidole Polisi, Magereza
January 31, 2023
Waliokutwa na meno ya tembo wahukumiwa miaka 20 jela (+video)
January 31, 2023
Maji ya ajabu yanayotoka bombani Johannesburg
January 31, 2023
Aa
Millard AyoMillard Ayo
Aa
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Search
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Follow US
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Millard Ayo > Blog > Breaking News > BREAKING: Mahakama ya Kisutu imemuachia huru Askofu Gwajima
Breaking News

BREAKING: Mahakama ya Kisutu imemuachia huru Askofu Gwajima

September 15, 2017
Share
2 Min Read
SHARE

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima na wenzake katika kesi ya silaha baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka.

Ni takribani miaka miwili na nusu ambapo leo September 15, 2017 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuachia huru Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima na wenzake katika kesi ya kushindwa kuhifadhi silaha na kuamuru Gwajima arudishiwe begi lake lenye risasi, bunduki na mali nyingine kwa sababu hakuna ushahidi kwamba alizembea kuhifadhi.

Mbali ya Gwajima, wengine waliochiwa huru ni mfanyabiashara anayedaiwa kuwa Mlinzi wake, George Mzava, Msaidizi wake, Yekonia Bihagaze na Mchungaji Georgey Milulu.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha amesema>>>”Nimelazimika kuwaachia washtakiwa wote kwa sababu kesi dhidi yao haijathibitika katika viwango vilivyotakiwa.”

Alisema kuwa ni wazi kwamba mshtakiwa wa kwanza ambaye ni Gwajima, aliripoti mwenyewe March 27, 2015 katika Kituo Kikuu cha Polisi kwa ZCO ambapo alifanya hivyo akiwa na begi lake mkononi, ambapo hadi anafika kwa ZCO alikuwa hakukaguliwa na askari yeyote.

Pia katika ushahidi wa kesi hiyo iliyokuwa na mashahidi 10, Hakimu amesema hakuna askari aliyeeleza kama Gwajima alifanyiwa ukaguzi kabla ya kuonana na ZCO ambapo alisema Jamhuri haikupinga kama Gwajima alizimia na kwamba alikuwa makini na timamu kuhakikisha yupo na bunduki na begi lake hata alipolazwa hospitali.

>>>”Hivyo nawaachilia washtakiwa wote kwamba kesi dhidi yao mashtaka hayajathibitika. Pia naamuru begi, risasi na mali zote za Gwajima zirudishwe kwake kwa sababu hakuna uthibitisho wowote katika hilo.”

Katika kesi hiyo inadaiwa kati ya March 27 na 29, 2015 Dar es Salaam, Gwajima alishindwa kuhifadhi silaha aina ya Beretta namba CAT 5802 , risasi tatu za pistol na risasi 17 za Short Gun.

Shtaka la pili na la tatu linawakabili washtakiwa waliobaki ambao wanadaiwa kwamba March 29, 2015 katika Hospitali ya TMJ Mikocheni ‘A’ walikutwa wakimiliki silaha na risasi hizo bila ruhusa kutoka mamlaka husika.

#BREAKING Mahakama imemuachia huru Gwajima na wenzake kesi ya silaha baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha #MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/kQwnZcW545

— AyoTV (@ayotv_) September 15, 2017

GWAJIMA AFUNGUKA ISHU YA LISSU KUPIGWA RISASI

You Might Also Like

Rais Samia ashtukia mchezo mchafu hela za Plea Bargain

Rais Samia ainyooshea kidole Polisi, Magereza

Waliokutwa na meno ya tembo wahukumiwa miaka 20 jela (+video)

Maji ya ajabu yanayotoka bombani Johannesburg

Biden akataa kutuma ndege za kivita Ukraine

TAGGED: Breaking news, TZA HABARI
Millard Ayo September 15, 2017
Share this Article
Facebook TwitterEmail Print
Share
Previous Article BREAKING: Polisi DSM waongea kuhusu mikusanyiko ya kumuombea Tundu Lissu na mengine
Next Article Mkutano wa Wakuu wa Polisi unaoendelea Uganda, IGP Sirro kahudhuria
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

You must be logged in to post a comment.

- Advertisement -

Latest News

Jorginho aondoka Chelsea na kusaini Arsenal
Sports February 1, 2023
Rais Samia ashtukia mchezo mchafu hela za Plea Bargain
Top Stories January 31, 2023
Rais Samia ainyooshea kidole Polisi, Magereza
Top Stories January 31, 2023
Waliokutwa na meno ya tembo wahukumiwa miaka 20 jela (+video)
Top Stories January 31, 2023

You Might also Like

Top Stories

Rais Samia ashtukia mchezo mchafu hela za Plea Bargain

January 31, 2023
Top Stories

Rais Samia ainyooshea kidole Polisi, Magereza

January 31, 2023
Top Stories

Maji ya ajabu yanayotoka bombani Johannesburg

January 31, 2023
Top Stories

Biden akataa kutuma ndege za kivita Ukraine

January 31, 2023
Show More
//

To be recognized as Africa’s leading and most trusted online media network providing quality content across all our media platforms by 2025

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

Millard AyoMillard Ayo
Follow US

© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.

Removed from reading list

Undo

Lost your password?