AyoTV

VIDEO: Hii kwa warembo watakaokwenda kuishangilia Taifa Stars Jumapili Taifa

on

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ya wachezaji wa ndani Jumapili ya Septemba 22 uwanja wa Taifa Dar es Salaam itacheza mchezo wake muhimu wa kuwania kufuzu kucheza fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN 2020) zitakazofanyika Cameroon.

Kuelekea mchezo huo ambao ni muhimu kwa Tanzania wanaoanzia nyumbani, kamati ya hamasa ya waandishi wa habari za michezo, imetangaza kugawa tiketi bure kwa wasichana watakao kuja Taifa wakiwa wamevalia jezi za Taifa Stars na wamechora bendera za timu ya taifa, watoto.

Lengo likiwa ni kuvuta watu wengi zaidi katika mchezo huo muhimu, kwani Stars inahitaji ushindi ili mchezo wa marudiano nchini Sudan utakaochezwa October 8, Taifa Stars iende kutafuta sare au ipoteze kwa idadi ndogo ya magoli endapo huku ikiwa imefunga mengi.

VIDEO: Moja kati ya magoli ya marehemu Jeba, hili liliwaumiza wana-Simba 2016

Soma na hizi

Tupia Comments