Top Stories

Kesi ya Vigogo CHADEMA: Askari adai alipigwa Jiwe kichwani, alitokwa damu (+video)

on

Tunayo stori kutokea kwa Askari Polisi namba H 7856 PC Fikiri Mgeta (28), ambapo ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa alilazwa siku tatu katika Hospitali ya Polisi Kilwa Road, baada ya kupigwa jiwe kichwani wakati wa maandamano ya viongozi CHADEMA.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Jacqueline Nyantori, shahidi huyo alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa alipigwa na jiwe kichwani pamoja na mkononi ambayo yalimuumiza na kusababisha kutoka damu nyingi. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 4 na 5, 2019 kwa ajili ya kuendelea na ushahidi.

ILICHOKISEMA TRA KUHUSU MABADILIKO YA SHERIA YA KODI “TUNA KIWANGO MFUTO”

Soma na hizi

Tupia Comments