Premier Bet
TMDA Ad

AyoTV

Msimamo wa Niyonzima ni upi anabaki au anaondoka? Meneja kaongea

on

Club ya Simba SC kwa sasa inamaliza msimu wa 2018/2019 huku ikiwa na mtihani wa kuboresha zaidi kikosi chao kwa kutaka kusajili wa wachezaji wapya na kuwaongezea mkataba wachezaji wake wanaomaliza mkataba, Haruna Niyonzima ni miongoni mwa wachezaji wa Simba SC ambao mikataba yao inaelekea ukingoni.

Kuelekea kumaliza mkataba wake AyoTV imeongea na meneja wa Haruna Niyonzima anayejulikana kwa jina la Roro Stratton kuhusiana na msimamo wao baada ya msimu kumalizika, Niyonzima vipi ataendelea kuwa na Simba SC? au kuna timu nyingine atatimkia.

“Ukiniuliza anaondoka au anabaki inakuwa kidogo ni swali ambalo halijakamilika kwetu sisi hapa kwa sababu Haruna hadi sasa hivi ana ofa takribani nne, asubuhi ya leo tumepata ofa kutoka South Africa kulikuwa na ofa tatu mbili zinatoka DRC kwa hiyo hatuwezi kusema kwamba ataondoka ama nini japo tumeshafanya mazungumzo ya awali na Simba SC”>>>Niyonzima

EXCLUSIVE: Msuva kuhusu kitendo cha Salamba kuomba viatu vya Banega

Soma na hizi

Tupia Comments