Habari za Mastaa

VARANGATI: Wolper amwambia Shilole “Unatudhalilisha” (+video)

on

Usiku wa Jully 9, 2019 Wasanii wa filamu nchini walikutana kwenye kikao cha wawekezaji wa kampuni ya ‘SwahiliFlix’ ambao wamekuja kuwekeza kwenye mauzo ya filamu na kazi za wasanii ambapo msanii Shilole aliibua zozo baada ya mzungumzaji wa kikao hicho kuonekana akitumia zaidi lugha ya kingereza ambayo msanii huyo alidai siyo wasanii wote wanaielewa.

Baada ya Shilole kumtaka mzungumzaji kutumia kiswahili kwa madai hayo kuwa siyo wasanii wote wanaelewa lugha ya kingereza ndipo muigizaji Wolper alipoingilia kati na kudai kuwa wanadhalilishwa kwenye kikao hicho.

Bonyeza PLAY hapa chini kutazama VIDEO ilivyokuwa.

VIDEO: Hatimaye wasanii walamba dili nono Steve Nyerere ahusika

 

Soma na hizi

Tupia Comments