Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

Simba SC imepata sare ya kwanza nyumbani Champions League vs TP Mazembe

on

Simba SC leo wamecheza game yao ya kwanza ya hatua ya robo fainali ya CAF Champions League dhidi ya TP Mazembe uwanja wa Taifa Dar es Salaam, Simba SC hii ilikuwa game yao ya 6 ya Champions League msimu huu kucheza uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Game hiyo TP Mazembe waliingia kwa tahadhari kubwa kutokana na Simba kutopoteza mchezo wowote ule wa CAF Champions League katika uwanja wa Taifa, Simba SC wameendeleza kucheza mchezo mzuri na kutengeneza nafasi lakini walishindwa kuzitumia na kupata sare 0-0.

Simba leo walikosa bahati licha ya kushambulia na kupata mkwaju wa penati uliopigwa na nahodha wao John Bocco ambaye alikosa, Simba watalazimika kwenda Lubumbashi weekend ijayo kucheza game ya marudiano, Simba ili atinge kucheza nusu fainali atahitaji sare ya kufungana magoli au ushindi wowote.

Ukimuuliza Mwinyi Zahera ishu za Ajib kurudi Simba SC….

Soma na hizi

Tupia Comments