Habari za Mastaa

Majani, Mwana FA na Mtitu waungana kuleta mapinduzi kwenye filamu (+video)

on

Wakongwe waungana kuleta mapinduzi kwenye filamu ambao ni Producer Majani wa Bongo records, msanii Mwana FA na mtayarishaji wa filamu Mtitu, kwa pamoja wameanza mchakato wa kuiandaa tamthilia mpya itakayouzwa kimataifa na kuwashirikisha mastaa tofauti tofauti.

Mastaa hao watakao shiriki kwenye tamthilia hiyo wanatarajiwa kutoka sehemu tofauti tofauti kuanzia kwenye filamu, muziki na hata wacheza mpira, huku usaili wa kuwapata ukitarajia kufanyika nchi tofauti ikiwemo Kenya, Uganda, Rwanda na Tanzania.

Hata hivyo tayari Mtitu, Majani na Mwana FA washaingia makubaliano ya kisheria kwaajili ya kuianza kazi hiyo na tayari wameandaa mikataba mizuri ya kisheria kwa washiriki wote watakao husika kwenye tamthilia hiyo ambayo usaili wake utaanza hivi karibuni.

Bonyeza PLAY hapa chini kutazam FULL VIDEO.

FULL VICHAMBO, UKITAKA KUVURUGA PENZI LA RIYAMA NA MUMEWE “USIHANGAIKE”

Soma na hizi

Tupia Comments