Kupitia mtandao wa TMZ umeripoti kuwa imekuwa ngumu kumpata mrithi wa Muigizaji Kevin Hart kwenye nafasi ya utangazaji wa tuzo za Oscars 2019 kutokana na malipo ya pesa kuwa madogo na hivyo watangazaji kukwepa nafasi hiyo.
Baada ya Kevin Hart kutangaza rasmi kuwa amejitoa ku-host tuzo hizo siku kadhaa zilizopita kutokana na sababu ya kuwakashfu watu wanaojihusiaha na mapenzi ya jinsia moja inaripotiwa imekuwa ngumu kumpata mtu wa kuchukua nafasi yake.
Inaelezwa kuwa mtangazaji maarufu Jimmy Kimmel aliwahi kulipwa kiasi cha zaidi ya Milioni 34 za Kitanzania ku-host sherehe ya tuzo za Oscars mwaka 2017 na wengi kudai kuwa kiasi hicho kilikuwa kidogo kutokana na ukubwa alionao mtangazaji huyo.
EXCLUSIVE: WEMA KAVUNJA UKIMYA, “MTOTO WANGU AVAE HIVI, ATOKEE HIVI”