Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba ametembelea mikoa mbalimbali Tanzania katika muendelezo wa ziara yake ya mazingira aliyoianza March 13 2017.
Moja kati ya sehemu alizotembelea Waziri Makamba ni Ngorongoro Crater ambako alijionea namna Bonde hilo maarufu lilivyokuwa na changamoto mbalimbali ikiwepo kuota kwa majani yenye sumu ambayo yanahatarisha maisha ya viumbe wanaoishi eneo hilo.
“Ngorongoro crater ni moja kati ya mbuga kubwa na nzuri duniani, lakini kuna jambo la kusikitisha kuhusu mbuga hii. Hivi karibuni kuna majani yenye sumu ambayo yameota sehemu kubwa ya mbuga hii na majani haya yamekuwa yakihatarisha maisha ya wanyama hasa wanaokula majani.” – January Makamba.
Bonyeza play kutazama…
VIDEO: Kwa nini January Makamba ameamua kukaa kimya kwenye mitandao ya kijamii? Bonyeza play kutazama.
BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millarday