Habari za Mastaa

Kylie Jenner atajwa kuwa tajiri wa kwanza duniani mwenye umri mdogo

on

Kwa mujibu wa jarida la Forbes limemtaja mfanyabiashara maarufu duniani Kylie Jenner kuwa ndiye tajiri mdogo zaidi duniani akiwa na umri wa miaka 21 na kumpiga chini Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Facebook MarckZuckerberg.

Inaelezwa kuwa bidhaa za urembo ( Kylie Cosmetics) zinafanya vizuri duniani kote ambapo mwaka 2018 bidhaa hizo zinatajwa kumuingizia Kylie Jenner kiasi cha dola za Kimarekani Milioni 360 na mwaka huu 2019 jarida hilo linataja kumuingizia zaidi ya shilingi Trilioni 2 za Kitanzania.

Ukiachilia mbali na Kylie Jenner kutajwa kama mfanyabiashara tajiri mwenye umri mdogo nchini Marekani  mwaka 2018 alitajwa na jarida la Forbes kushika nafasi ya tano katika list ya watu Maarufu wenye utajiri mkubwa nchini humo huku akiambatana na rapper Jay Z.

 

PERFECT CRISPIN: “BILA RUGE NISINGEKUWA HAPA, ALIPENDA TUPIGANE”

Soma na hizi

Tupia Comments