Serikali ya Nigeria kupitia Shirika la Utangazaji la Taifa (NBC) limefungia baadhi ya nyimbo za Mastaa wa Afrika zikiwemo nyimbo mbili za Davido.
Katika list iliyotolewa na Shirika hilo, imezitaja nyimbo tano ambazo hazitoruhusiwa kuchezwa katika vituo vya Television wala kupigwa kwenye Radio kwa sababu ya kukiuka maadili.
Nyimbo hizo ni pamoja na ‘Fall’ na ‘If Remix’ za Davido, nyimbo ‘Wo’ na ‘Wavy Lines’ za Olamide na ‘Living Things’ wa 9ice.
Wizara ya Afya kupitia tweet ilisema kwamba video ya wimbo ‘Wo’ wa Olamide ina sehemu ambayo inawaonesha watoto wakivuta sigara ikiwa ni kinyume cha taratibu ambapo kwa mujibu wa Mamlaka, inakinzana na Sheria ya Tumbaku ya mwaka 2015 ambayo inakataza matumizi ya tumbaku kwa wenye umri wa chini ya miaka 18.
Hata hivyo, Mamlaka hayo hayajaweka wazi kuhusu kuzifungia nyimbo za Davido lakini inadhaniwa ni kwa sababu NBC inataka kulinda kazi na maudhui kwenye video na nyimbo za Nigeria.