Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Makumbusho ya Madame Tussauds imegoma kutoa sanamu la Michael Jackson

on

Leo March 21,2019 fahamu kuwa eneo la makumbusho ya Madame Tussauds lililopo jiji la London nchini Uingereza limeweka wazi kuwa halitaondoa sanamu lolote la Mfalme wa Pop Marehemu Michael Jackson kufuatia skendo ya ulawiti inayoendelea kwa sasa.

Kutokana na makumbusho hiyo kuhifadhi kumbukumbu za watu maarufu mbalimbali ambao wana mchango mkubwa kwenye tamaduni na wageni huvutiwa na kutarajia kuwaona katika makumbusho hiyo basi msemaji wa makumbusho amesema kuwa taasisi yao haitofanya zoezi la kulitoa sanamu la Mfalme huyo wa Pop hata kwa baadae.

Hivi karibuni sanamu ya Michael Jackson iliondolewa kwenye makumbusho ya taifa ya mpira wa miguu nchini Uingereza kufuatia tuhuma hizo na inaripotiwa kuwa sanamu hilo lilikuwepo tangu mwaka 2014.

VIDEO: BIFU!! AMBER LULU NA HAITHAM WATIBUANA, ADAIWA KUIBA MUME

Soma na hizi

Tupia Comments