Inaripotiwa kuwa mlinzi wa zamani wa marehemu Michael Jackson ameibuka na kumkingia kifua baada ya tuhuma za ulawiti dhidi ya wavulana wadogo zilizokuwa zikimuandama zilizotolewa na waathirika Wade Robson na James Safechuck.
Inaelezwa kuwa Bill Whitefield ameandika kitabu ambacho kinachosimulia muda wake na Marehemu Michael Jackson baada ya kumfanyia kazi ya kumlinda kwa miaka miwili. Bill amefanya mahojiano na podcast ya ‘Hidden Truth Show with Jim Breslo’ na kusisitiza kuwa MJ hakuwahi kuhusika na vitendo vya ulawiti bali alikuwa akivutiwa sana na wanawake (heterosexual) walijadili sana masuala ya wanawake muda mwingi
Bill aliongeza kwa kusema kuwa MJ alikuwa akivutiwa na stori za wanawake, hivyo anashangazwa na taarifa za vitendo vya ulawiti zinazoendelea hasa kupitia makala fupi ya ‘Leaving Neverland’ iliyoachiwa na televisheni ya HBO.
“MJ alikuwa akizungumzia zaidi wanawake hata wakati tukiwa tunaendesha gari nakumbuka kuna siku aliomuona msichana mrembo na alishusha kioo cha kwenye gari na kumsifia nilimuuliza unamtaka? alinijibu kwa aibu na kusema hapana” >>>Bill Whitefield
VIDEO: NOMA!! HII NDIYO LAST MINUTE YA IRENE UWOYA INABEBA WATU 300