Stori Pekee

Umewahi kulala hotelini kisha ukatoka na kuacha funguo za chumba reception? jamaa mmoja kamtega muhudumu na camera

on

LodgeWengi wetu tumekuwa tukisafiri kwenda sehemu mbalimbali na kufikia katika nyumba za wageni, tumekuwa na imani nazo sana katika masuala ya usalama wa vitu vyetu lakini unajua ambacho huwa kinaendelea nyuma iwapo unakuwa umetoka na kuacha funguo za chumba chako kwa mhudumu wa mapokezi?

Sasa jamaa mmoja aliyefikia katika moja ya nyumba za wageni Marekani, alitoka na kuacha kamera ya laptop yake ikiwa inarekodi video ya kila kinachoendelea ndani ya chumba alichofikia kwenye guest hiyo, kilichoonekana kwenye video hiyo mhudumu aliyeingia kufanya usafi alionekana kuwa huru na vitu vya mteja wa chumba hicho na alionekana akipekua kila kitu kwa amani kabisa!

Hizi ni picha kutoka kwenye video hiyo ambayo imeenea katika mtandao wa Youtube zikimuonyesha mhudumu huyo akipekua vitu vya mteja wa chumba hicho.

Hotel CleanerHii ni tahadhari kwa wale watu wangu wote ambao huwa wanajiachia sana wakiamini baada ya kukabidhiwa chumba wewe ndio mmiliki pekee, kuacha hela, laptop na vitu vingine ovyo…

Hapa alikuwa anacheki listi ya mizigo aliyoipokea mteja wa chumba hicho.

Hapa alikuwa anacheki listi ya mizigo aliyoipokea mteja wa chumba hicho.

Alianza kwa kushangaa game ya PS3 aliyoiacha teja wa chumba hicho.

Anashangaa game ya PS3 aliyoiacha mteja wa chumba hicho.

Hapa alikuwa anacheki listi ya mizigo aliyoipokea mteja wa chumba hicho.

Hapa alikuwa anacheki listi ya mizigo aliyoipokea mteja wa chumba hicho.

Umewahi kukumbana au kusikia tukio lolote kama hili? kuacha chumba chako na kurudi ukakuta kimepekuliwa? ilikuaje?

 Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Tupia Comments