Michezo

Baada ya Mbrazil Firmino, Liverpool sasa inajipanga kumchukua huyu mwingine !!

on

  Baada ya Klabu ya Liverpool kufanikisha usajili wa Danny Ings kutoka Burnley na Roberto Firmino kutoka Klabu ya Hoffenheim ya Ujerumani, Klabu hiyo sasa hivi iko njiani kuhakikisha inakamilisha usajili mchezaji mwingine ndani ya saa chache zijazo.
Taarifa kutoka vyombo vya habari vya England, Liverpool wamefanikiwa kutuma ofa ambayo imekubalika tayari Southampton kwa ajili ya kumsaini beki wa kimataifa, Nathaniel Clyne.

Liverpool walituma ofa ya Paundi Milioni 12.5 kwa ajili ya Clyne, na baada ya Southampton kuikubali sasahivi kilichobakia ni suala la vipimo vya afya ili mchezaji huyo ajiunge na Kikosi hicho.

Clyne ambaye yupo katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake na Southampton kwa sasa yupo mapumzikoni na anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka 5 ikiwa atafuzu vipimo vya afya.

Pozi la Roberto Firmino baada ya kusaini Liverpool

Kama usajili ukikamilika mchezaji huyu atakuwa mchezaji wa sita kusajiliwa na Liverpool katika dirisha hili la usajili, ambapo ataungana na Firmino aliyetua Anfield kwa ada ya Paundi Milioni 29… Wachezaji wengine waliosajiliwa ni James Milner, Adam Bogdan na Joe Gomez.

Jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments